Kuhakikisha ufungaji wa vifaa vyako ya satelaiti unafanyika kwa usahihi ni hatua muhimu baada ya kuhakiki upatikanaji wa huduma katika eneo unalotaka kufunga huduma ya mtandao wa kasi wa mfumo wa satelaiti kwa matumizi ya nyumbani au ofisi. Kuna mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kufunga vifaa vya huduma ya intaneti ya satelaiti.
Hakikisha ufungaji wa vifaa vyako vya satelaiti unafanywa na mtaalamu
Maduka yetu na washirika wetu hupanga ufungaji ufanywe na mtaalamu wa ufungaji wa vifaa vya satelaiti. Wamefundishwa kuhakikisha kifaa kimeweka sehemu sahihi na kuhakikisha ungo umeelekezwa kwa usahihi kuweza kuwasiliana na satelaiti ya Konnect. Hii inahakikisha unapata huduma bora zaidi ya intaneti kutoka angani.
Chagua mahali ambapo kifaa cha satelaiti kinapaswa kufungwa
Mtaalamu wa ufungaji huduma atakupa ushauri kuhusu eneo bora zaidi la kufunga dish la kupokea intaneti ya satelaiti.
Sehemu lazima iwe:
- Kwenye eneo lisilohama kama vile ukuta, paa au ardhi, haiwezi ikawa kwenye gari inayotembea, au kufungwa kwenye miti.
- Eneo linatakiwa liwe lenye kuona anga ili kufikia Satelaiti ya Konnect, bila uwepo wa kizuizi chochote kama vile miti au majengo. Unaweza tumia app ya Konnect Sat Finder ili kuhakiki.
Kuwa tayari kwa siku ya ufungaji
Ungo na kifaa cha upokeaji vitafungwa nje ila modem itafungwa ndani ya nyumba au ofisi yako. Fikiria ni eneo gani la nyumba ungetaka modem ifungwe, unashauriwa kuchagua eneo utakalokuwa unatumia huduma zaidi. Mfungaji ataunganisha modem yako na kukuonesha jinsi ya kuingia kwenye mfumo wa wateja wa Konnect (Konnect Customer Portal) unaokuwezesha kuona na kusimamia matumizi yako ya data.
Baada ya ufungaji
Timu ya huduma ya Wateja ya Konnect ipo tayari kukusaidia na maswali yote utakayokuwa nayo ili kukuwezesha kupata huduma iliyobora kutokana na ufungaji wa intaneti mfumo wa satelaiti, na timu ipo kwa ajili yako utakapoihitaji iwapo utakutana na changamoto zozote za huduma.