Intaneti ya mfumo wa satelaiti ina faida ya kufikia eneo kubwa zaidi na hivyo kuweza kuunganisha familia na biashara nyingi ambazo zinahitaji huduma ya intaneti ukilingana na huduma zingine za intaneti za ardhini kama za faiba.
Unaweza kushiriki kwenye Zoezi la upatikanaji wa huduma ili tuweze kuhakiki sifa ya eneo unalotaka kufunga huduma kama tayari linafikiwa na huduma yetu ya intaneti yenye kasi ya mfumo wa satelaiti.
Kutegemeana na eneo ulilopo unaweza kuhitaji kifaa cha aina tofauti ili kuhakikisha ubora wa huduma ya intaneti ya mfumo wa satelaiti kukufikia kwa uhakika.
Fanya zoezi la kutambua upatikanaji na ufikiwaji wa huduma ya intaneti ya satelaiti nchini Tanzania
Jinsi eneo unalotaka kufunga huduma linaweza kuathiriwa na upatikanaji wa intaneti ya satelaiti
Ukishafanya majaribio ya upatikanaji wa huduma katika eneo unalotaka, kuna mambo mengine pia ya kuzingatia.
Ili kuweza kupokea huduma ya intaneti kutoka kwenye satelaiti iliyo angani, dishi lako halitakiwi kuzibwa na kitu chochote, linatakiwi liweze kuangalia angani usawa wa satelaiti yetu bila kuwa na kizuizi chochote. Kama eneo ulilofunga vifaa basi lipo kwenye bonde kali, lililozungukwa na vilima, unaweza kosa huduma ingawa upo eneo ambalo tayari tunalifikia kwa huduma ya Konnect. Pia mfano kama ulipo funga vifaa ni karibu na majengo marefu yanayozuia dishi kupata nafasi nzuri, huduma pia inaweza athirika katika kukufikia. Usisite kuangalia dondoo muhimu za jinsi ya kufunga vya huduma ya intaneti ya satelaiti.
Ni muhimu kufahamu kwa ujumla huduma haiathiriwi na mabadiliko ya hali ya hewa. Ila tambua, kama mabadiliko ya hali ya hewa ni makali sana kama vile mvua kubwa zenye upepo mkali n.k zinaweza athiri huduma kwa muda mfupi. Upepo mkali unaweza sogeza dishi na kulifanya litazamo upande usio sawa na upande ambapo satelaiti inatazama, na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma. Ila hali hizi ni nadra sana kujitokeza na mafundi wetu waliobobea wataweza kukusaidia na kukurudishia huduma mapema iwazekanavyo kama hali hiyo ikijitokeza.